HIKI NDICHO KINACHO MKERA ZAIDI IRENE UWOYA KWENYE MITANDAO YA KIJAMII - BZONE

HIKI NDICHO KINACHO MKERA ZAIDI IRENE UWOYA KWENYE MITANDAO YA KIJAMII

Share This
ENTERTAIMENT: Msanii wa Bongo movie Irene Uwoya, amezungumzia vitu ambavyo vinamchukiza sana kwenye mitandao ya kijamii hasa Instagram. Muigizaji huyo amesema anachukizwa na watu ambao wanaamini matusi ndio kila kitu.
“Unajua sisi mashabiki zetu wapo katika nafasi  ya kusema kama tunakosea au tunapatoa, lakini njia wanayoitumia kutuelewesha sio nzuri,” ameiambia Dizzim Online.
“Wao wanatumia matusi badala ya kumwambia mtu taratibu akaelewa. Halafu wanasahau kwamba wasanii ni binadamu kama binadamu wengine, so tunavyoishi tunaishi kama watu wengine tu. Msanii sio malaika, saa zingine hawajui mtu unakuwa katika hali gani, labda umefiwa au unaumwa wao wanatukana tu,” amesisitiza.
Ameongeza, ” Pia watu wanaohack account, unakuta mtu ana followers wengi sana kapata shida sana kupata halafu mtu anatoka huko anakuja kuhack, nakerwa sana.”
Hivi karibuni muigizaji huyo amesaini deal la ubalozi na kampuni ya utengenezaji simu ya Asia.

No comments:

Post a Comment

Pages