SPORTS: KLABU ya Singida United imefanikiwa kukamilisha usajili wa mshambuliaji wa zamani wa Yanga, Atupele Green Jackson kutoka JKT Ruvu ya Dar es Salaam.
Taarifa ya Singida United imesema mchezaji huyo amesaini mkataba wa miaka miwili usiku wa Jumatatu na Jumanne mchana anatarajiwa kutambulishwa rasmi.
Atupele anajiunga na Singida United baada ya klabu yake, JKT Ruvu kushuka daraja katika msimu ambao alijiunga nayo kutoka Ndanda FC ya Mtwara.
Atupele ni mfungaji bora wa Kombe la Shirikasho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) mwaka jana, kabla ya mwaka huu kupokonywa na heshima hiyo na Mzambia, Obrey Chirwa wa Yanga.
Na kumsajili Atupele ni mwendelezo wa Singida United kusajili wachezaji nyota wa nyumbani na nje ya nchi ili kutengeneza kikosi kikali cha ushindani msimu ujao.
Tayari Singida iliyopanda Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara inaye kocha mzoefu, Mholanzi Hans van der Pluijm iliyemchukua Yanga.
Home
Unlabelled
ATUPELE GREEN ATUA SINGIDA UNITED MIAKA MIWILI
ATUPELE GREEN ATUA SINGIDA UNITED MIAKA MIWILI
Share This
Share This
About Bwherever
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Author Details
Bwherever is a Tanzanian Radio Personality and Blogger who initiative Bbaseonpoint blog.
No comments:
Post a Comment