AFUNGIWA KISA KUMBUSU MWANDISHI WA HABARI - BZONE

AFUNGIWA KISA KUMBUSU MWANDISHI WA HABARI

Share This
SPORTS: Mchezaji wa Tenisi Maxime Hamou amefungiwa kushiriki michuano ya French Open mjini Paris, baada ya kujaribu kumbusu mwandishi wa habari mara kadhaa wakati wa mahojiano.
Mfaransa huyo mwenye miaka 21 alijaribu kumbusu Maly Thomas huku akiwa amemshika mabega yake na shingo licha ya mwanadada huyo kukataa mara kwa mara. Alikuwa akihojiwa siku ya jumatatu baada ya kupoteza mchezo wake katika mzunguko wa kwanza.Hamou katikati akiwa ameinama kumbusu Maly Thomas
Katika taarifa yake, chama cha Tenisi nchini Ufaransa kimesema kitendo hicho ni cha kukemewa kwa nguvu.

No comments:

Post a Comment

Pages