ROMA, WENZAKE KUSIMULIA KUHUSU TUKIO ZIMA LA KUTEKWA KWAO LEO - BZONE

ROMA, WENZAKE KUSIMULIA KUHUSU TUKIO ZIMA LA KUTEKWA KWAO LEO

Share This
ENTERTAIMENT: Msanii wa muziki wa hip hop, Roma Mkatoliki, Moni pamoja na wenzao 2 leo wanatarajiwa kueleza sakata zima la tukio la kutekwa kwao wakiwa studio za Tongwe Records Masaki, jijini Dar es Salaam.
Wasanii wanaodaiwa kutekwa ambao wataungana na Roma katika mkutano na waandishi wa habari leo ni Moni Centrozone, prodyuza wa studio hiyo, Bin Laden na mfanyakazi wa mama mzazi wa mmiliki wa studio hiyo, Junior Makame (J Murder), anayefahamika kwa jina la Imma.
Juzi usiku baada ya kuruhusiwa kutoka Kituo cha Polisi Oysterbay, Dar es Salaam na kufanyiwa uchunguzi katika Hospitali ya Mwananyamala, Roma aliwaambia waandishi wa habari kwamba atazungumza leo.
“Mi ni mzima kabisa, nipo vyema kiafya na kiakili na wenzangu watatu nikimaanisha Mon, Bin Laden prodyuza wetu pamoja na Imma mfanyakazi wetu pale Tongwe; wote tu wazima tunaendelea vizuri, kwa sasa tupo katika taratibu za kutoa taarifa za tukio zima ambavyo limetokea.
“Lakini taratibu hizo zinatufunga tusiweze kuongea chochote kwa sasa hivi, lakini ratiba naweza kuwapa kushinda kesho Jumapili, Jumatatu nadhani ndiyo kutakuwa na ‘Press Conference’ kukutana na kuongelea kuhusu hiyo stori, mturuhusu tu tukapumzike nawashukuru, niseme tu asante,” alisema Roma.
Roma na wenzake walitekwa Jumatano wiki hii wakiwa katika studio za Tongwe Recods iliyopo Masaki jijini Dar es Salaam.
Baki na sisi upate update zote za tukio zima.

No comments:

Post a Comment

Pages