JE WAJUA NI KWANINI KAMBA ZA VIATU HUFUNGUKA ZENYEWE - BZONE

JE WAJUA NI KWANINI KAMBA ZA VIATU HUFUNGUKA ZENYEWE

Share This
Wamebaini kuwa nguvu ya miguu kukanyaga ardhi, huvuta na kisha hulegeza kifundo cha kamba kilichofungwa,LIFESTYLE: Sasa wanasayansi wanadhani kuwa, wanajua sababu, ya vifungo hivyo kufunguka.
Wamebaini kuwa nguvu ya miguu kukanyaga ardhi, huvuta na kisha hulegeza kifundo cha kamba kilichofungwa, sawa na mkono usioonekana, ukifungua kamba hizo taratibu.
Watafiti wanasema kuwa uelewa huu wa namna kamba za viatu hufunguka, uko sambamba na namna DNA inavyofanya kazi.
Kwa kutumia camera inayonasa na kuwasilisha picha kwa mwendo wa pole, na mfululizo wa majaribio, wahandisi wa mitambo katika Chuo Kikuu cha California Berkley, wamepata kuwa "kushindwa kwa kifungo cha kamba" hufanyika kwa sekunde kadhaa, inayochochewa na nguvu kadha wa kadha.Utafiti huo ulianza kwa ushirikiano wa uasisi na mwanafunzi mmoja wa chuo kikuu
Mtafiti mkuu Christopher Daily-Diamond, anasema kuwa: "unapozungumzia aina ya vifundo, ikiwa utaweza kuanza kuelewa kamba ya viatu, bila shaka utatumia mbinu hiyo hiyo, kwa vitu kadhaa, kama vile DNA au namna kitu kinapojiunda na kuweza kuonekana tu kwa uwezo wa mtambo wa microscope, chini ya nguvu imara.
"Hii ni hatua ya kwanza kuelewa, namna vifungo vingine huwa bora kuliko vingine, ambayo hakuna mtu ambaye amewahi kufanya."
Utafiti huo ulianza kwa ushirikiano wa uasisi na mwanafunzi mmoja wa chuo kikuu Christine Gregg, alifunga viatu vyake vya kukimbilia na kufanyia mazoezi kwenye kifaa cha eneo la mazoezi au Gym, huku mwanafunzi mwenzake akipiga picha ya video.
Kutokana na nguvu hiyo, kifundo hicho hujinyosha na kujikunja tena.

No comments:

Post a Comment

Pages