Diamond Platnumz Acha Nikae Kimya - BZONE

Diamond Platnumz Acha Nikae Kimya

Share This
ENTERTAIMENT: Diamond amepiga style za Beyonce, kuachia ngoma kwa kushtukiza. Wimbo huo uitwao Acha Nikae Kimya unazidi kwenda viral kutokana na ujumbe uliomo ikiwemo kumtetea mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

Kama bado hujausikia, haya ni mashairi yake niliyokuandikia:
Nasema walau nina kidogo na mashabiki wananiambia mbona hausemi chochote
Ah, si uko nao siku zote ama ulezi unafanya uogope
Ah na media pande zote wanalalama kiongozi atoke
Ah nchi inaingia matope niende wapi na mimi mtoto wa wote,
Yaani lawama, acha nikae kimya, niongee, kimya (ooh ninyamaze mimi)
Nikae kimya nisemee (kimya) mama kaniambia (acha nikae kimya)
Ooh nifunge m[u]domo, mimi bado m[u]dogo nisiseme (kimya)
Verse
Ni mengi majaribu najaribu kuepuka yasije nicost
Japo mengine swadakta mengine hayana maana
Rafiki kipenzi wa karibu hata nyimbo yake sikuweza ipost
Ila alipokamatwa iliniumiza sana mitandaoni kila kona
Uongo na ukweli unashonwa kila nyumba inanong’ona, ahh, ooh Tanzania
Mara kibembe Dodoma wabunge pinzani wamegoma juzi akapotea na Roma
Ohh Tanzania
Najaribu kunyamaza Makame hataki ohh ananiambia walau nina kidogo
Nyumbani nafungwa geti niende kwa Mangi kununua super gate
Napewa za chini ya kapeti kuna redio imevamiliwa eti
Ehh, napita kwenye magazeti nakuta lundo la watu wameketi
Ehh badala ya kutafuta senti wanabishana tu mambo ya vyeti
Acha nikae kimya (nisiongee ) nikae kimya (ninyamaze kabisa)
Nikae kimya (ulimi koma) kimya (usije kuniponza) acha nikae kimya
(nifunge bakuli langu) nikae kimya (nikojoe nikalale) kimya
Mimi bado mdogo sana mama kanimbia
Bridge
Najiuliza wapi (wapi) najiuliza wapiii, tunakwenda wapi
Wapi, kila siku maneno, wapii, hatuwajengi jamaa
Mimi na wewe ni taifa moja, Kambarage baba mmoja
Sasa tofauti za nini tushikamane tukaijenge Tanzania

No comments:

Post a Comment

Pages