HAWA NDIO MAREFA WATAKAO CHEZESHA MECHI YA LEO STARS NA LESOTHO - BZONE

HAWA NDIO MAREFA WATAKAO CHEZESHA MECHI YA LEO STARS NA LESOTHO

Share This
SPORTS: Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), limetangaza wamuzi wa mchezo kati ya Tanzania na Lesotho unaotarajiwa kufanyika Leo Jumamosi, Juni 10 mwaka huu kwenye Uwanja wa Azam Complex ulioko Chamazi, Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa CAF, waamuzi hao ni Abdillah Mahamoud, ambaye ni mwamuzi wa kati huku wasaidizi wake ni Gamaladen Abdi na Farhan Bogoreth wakati mwamuzi wa akiba atakuwa Twagirumukiza Abdoulkarim kutoka Rwanda huku Kamishna akiwa ni Amir Hassan wa Somalia.

Mchezo kati ya Taifa Stars na Lesotho, utafanyika kuanzia saa 2.00 usiku kwenye Uwanja wa Azam uliko Chamazi, Dar es Salaam. Mchezo huo dhidi ya Lesotho utakuwa ni wa kwanza kwa Taifa Stars katika Kundi ‘L’ kuwania nafasi muhimu ya kucheza fainali za Kombe la Mataiafa ya Afrika (AFCON) za mwaka 2019 zitakazofanyika nchini Cameroon.
Mbali ya Lesotho na Tanzania, Mataifa mengine katika Kundi ‘L’ ni Uganda na Cape Verde ambao pia wikiendi ya Juni 9, 10 na 11, watakuwa katika michezo yao ya kwanza pia kuwania nafasi hiyo.

No comments:

Post a Comment

Pages